Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limezindua uuzaji wa tiketi za safari ya kwanza kabisa ya ndege zake za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Marekani.
Shirika hilo linapanga kufanya safari yake ya kwanza mnamo 28 Oktoba, hatua itakayoifanya Kenya Airways kuwa shirika la kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa na safari za moja kwa moja Marekani.
Ndege za shirika hilo litakuwa zinafasiri moja kwa moja hadi uwanja wa ndege wa JFK, New York.
Tiketi za kawaida zinauzwa Sh89,000 za Kenya
pia ($890) za kimarekani