simu wa klabu ya Chelsea, kwa mujibu wa beki wa klabu hiyo Cesar Azpilicueta.
Amesema hayo huku ikionekana wazi kwamba itakuwa mwujiza kwao kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Hii ni baada yao kutoka sare ya 1-1 West Ham na hivyo kudidimiza zaidi matumaini ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi Kuu ya England msimu huu.
Kutoka sare kwa timu hiyo Jumapili kumeiacha Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Premia wakiwa pointi 10 nyuma ya Liverpool na Tottenham katika nafasi ya tatu na ya nne.
Msimamo wa ligi ya EPL 2017/18
Bao la kusawazisha la Javier Hernandez la kipindi cha nusu ya pili ya mchezo liliinua matarajio ya West Ham ya kuendelea kubakia katika michuano ya Ligi ya Premia dakika ya 73 lakini likawaumbua Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge.
Cesar Azpilicueta aliifungia Chelsea bao lake la tano la Ligi ya Premia dhidi ya West Ham akicheza mechi yake ya 191
Inamaanisha kuwa huenda wasifuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
"Tuko nyuma sana," alisema Azpilicueta, aliyekuwa amefungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 36.
''Ni kauli kubwa na kwa kiasi fulani aliyoitoa Azpilicueta... nimeipenda, anajivunia klabu yake na anafahamu fika malengo ya Chealsea, na kutoa kauli hiyo inamaanisha kuwa amevunjika moyo kwa mahala walipo sasa,'' alisema mchanganuzi wa mechi za siku Jermaine Jenas katika mazungumzo na BBC.
Mustakabali wa kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte haueleweki baada ya timu yake kuteteleka katika msimu huu wa Ligi ya Premia
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho alifutwa kazi wakati wa msimu wa mwaka 2015-16, wakati timu hiyo ilipomaliza ikiwa katika nafasi ya 10 katika Ligi ya Premia.
Na maswali pia yanaibuka juu ya mustakabali wa kocha wa sasa Antonio Conte, ambaye ameongoza timu hiyo baada ya kushinda taji mwaka jana.
Huku zikiwa zimesalia mechi sita, kihesabu Chelsea inaweza kufika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ingawa itabidi timu za Liverpool (ambao wamesalia na mechi tano) na Tottenham (ambao bado wana mechi sita za kucheza) ziporomoke.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema yeye ni raia wa Tanzania na yule “anayesema mimi sio raia wa Tanzania aniambie ni raia wa nchi gani.
Askofu Kakobe ametoa kauli hii Jumatatu baada ya kutoka kuhojiwa ofisi ya uhamiaji ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa takriban saa tatu.
Amesema inawezekana kuwa uhamiaji ina nia njema, lakini amehoji ni “kwa nini sasa, kwa nini wanahojiwa watu fulani wa kutoka eneo fulani la Kigoma. Mbona hatujasikia watu kutoka Dodoma, Kaskazini wakihojiwa.”
Vyanzo vya habari vimesema kuwa Askofu Kakobe ametakiwa kuacha hati yake ya kusafiria ili iweze kuwasaidia kupata taarifa zake muhimu huku yeye akisisitiza “hiki wanachokifanya kina tia shaka.